Karibu nikufundishe kutengeneza udi wa harusi,udi wa sukari,udi wa unga,udi wa kuogea na udi aina mbalimbali, utakaotengeneza kwa mkono wako nyumbani kwako mwenyewe,,ambapo utajiwezesha kuingiza kipato zaidi ya laki tatu kwa mwezi,kwa ada ya sh elfukumi tuu,pia utakapojiunga nitakufundisha njia za kutengeneza natural max,natural scrub,natural steaming na natural facial, nakupa pia offer yakukufundisha kutengeneza shampoo bure kabisa,,ntakupa pia mafunzo yakupika PIZZA,BURGER,PUDDING,EGGCHOP NA MITRO bure kabisa,wahi nafasi darasa linaanza muda si mrefu,,kwa nini ulalamike maisha magumu mkombozi wako nipo??kwa maelezo zaidi njoo whttsp no0778138742 au follow instagram@naima_kimwanya@naima_kimwanya
Wednesday, 17 May 2017
Sunday, 14 May 2017
Tambua mambo muhimu ili kuimarisha afya yako.
Naomba nikujuze mambo matano muhimu yakuimarisha afya yako ila kumbuka awali ya yote mazoezi ni muhimu kwa afya yako.
1. unaishi sehemu yenye baridi kali unataka uhisi joto? lamba asali kijiko kimoja halafu unaweza ukachemsha tangawizi ukanywa, tumai muda mwingi tumia kusugua viganja vyako vya mikono na uviweke mashavuni.
2. Unahisi maumivu ya viungo? miguu, mikono, mgongo n.k? chemsha bamia bila chumvi kunywa, pia pendelea kula kijiko kimoja cha asali kilichochanganywa na mdalasini
3. Kichwa kinauma sana? kata ndimu kipande na ujisugue paji la uso, kunywa maji kwa wingi,chemsha chai ya rangi yenye majani mengi kunywa na kwa wadada epuka kuvaa vilemba vyeusi kichwani.
4. Una tatizo la kusahausahau? pendelea kunywa juice ya mabungo, chemsha bilinganya tia tangawizi, nyanya, kitunguu na chumvi kidogo kula kama mboga,hii pia ni nzuri kwa wanaosumbuliwa na vidonda vya tumbo.
5.Unamatatizo yakusinzia mara kwa mara? chemsha kahawa tia iliki na rose water kidogo sana, kunywa kutwa mara tatu, hii pia ni nzuri kwa vile inatibu maradhi ya ini na figo na kwa wale madj, na wafanyakazi waendao shift ya usiku ni nzuri pia, natumai umenielewa, jitahidi kutenga muda kwa ajili ya kulala ili kuipumzisha akili japo masaa mawili kwa mchana kwa wale wasio na kazi,na kwa waendao makazini basi hakikisha usiku unalala si chini ya masaa manane.
Usisahau kutufuata instagram @pmgtanzania
Sunday, 23 April 2017
Hivi unajua jina Bluetooth limetokana na nini?
Kwa karne hii ya 21 ni njia rahisi sana inayo mwezesha mtu kuweza kuhamisha mafaili(data) kutoka kifaa kimoja kwenda kwenye kifaa kengine.
Mnamo mwaka 1966 Bwana Jim Kardach mmoja kati ya waanzlilishi wa teknologia hiyo ya bluetooth alikuja na jina hilo wakati walipo kuwa wakipiga strory na wenzake zakihistoria.
Msemaji mkuu wa club ya Simba Haji Manara asimamishwa kujihusisha na masuala na mpira wa miguu
Kamati ya maadili ya TFF Leo imetoa hukumu kwa Msemaji wa Simba Sports Club, Haji Manara kufuatia kutokuitikia wito wa kamati hiyo.Kamati hiyo imetoa hukumu ya makosa matatu dhidi ya Manara na hatimaye kumtoza faini ya Tsh. Milioni 9 pamoja na kutokumruhusu kujihusisha kwa shughuli za mpira wa miguu.
Mambo ya Kufanya Pale Simu au Tableti Yako Ikilowa au Kuingia Kwenye Maji
Mara nyingi jambo la kwanza atakalofanya mtu ni kuhangaika kufuta maji hayo mara moja…. iwe kwa kutumia nguo yake, au chochote kile cha karibu. Ila je ni sahihi? hapana!
Itoe mara moja kwenye maji. Inavyozidi kukaa kwenye maji muda mrefo ndivyo uwezekano wa kupona katika janga hili unakuwa mdogo zaidi. Imedondoka kwenye choo? Hapo itakubidi ufanye maamuzi ya haraka kama utaichomoa haraka au uisahau kabisa. Utafanya nini?
Bila kupoteza muda izime mara moja! Na kama ni simu yenye eneo la kutoa betri basi usitumie switchi yake kuzimia, bali toa betri mara moja. USIJARIBU KUBONYEZA KINGINE CHOCHOTE, ONDOA BETRI. Na kama ni tableti au simu za iPhone ambazo hazina sehemu za kutolea betri bofya eneo la kuzimia mara moja.
LENGO: Ni kuzima simu au tableti hiyo kabla hakujatokea shoti ya aina yeyote, kama simu imeingia maji alafu ukaifuta na kuanza kujaribu kuichezea kwa kubofya unaweza sababisha shoti inayoweza ikaiua simu yako mara moja.
Ifute taratibu. Kwa kutumia kitu kama taulo lililo kavu, angalia kwa ukaribu maeneo kama vile ya kuweka waya wa ‘earphones’, hakukisha pameacha kutoa maji. Puliza maeneo ya matundu kuhakikisha maji yameisha kabisa ndani. Pia toa vitu kama vile kadi ya laini, memori kadi na betri, kava, vikaushe pia.
Usitumie njia za ajabu kama vile kuiweka kwenye oveni ili kuikausha…joto la oveni ni kali sana utaua simu yako. 🙂
Njia A: Unavijua vipakti flani hivi vidogo vinakuwaga kwenye viatu vipya? Vinaitwa “silica gel packets”, ndani yake inavidonge vidogo vya Silica. Kama unavyo au unaweza kuvipata basi chukua mfuko wa plastiki unaoweza kuufunga kuzuia hewa, weka simu yako na vipakti hivyo katika mfuko huo kisha ufunge.
Njia B: Kama njia A haiwezekani basi fuata njia hii, zungushia simu yako kwenye tishu (Toilet Paper/Napkins) kisha iweke kwenye chombo ulichoweka mchele wa kutosha kuifunika kabisa. Mchele unasifa ya kunyonya unyevunyevu kama vile kwenye njia A. Unazungushia tishu ili kuondoa uwezekano wa simu yako kuingiwa na vumbi la mchele.
Baada ya kufanya tulichoongelea katika hatua ya 4 itakubidi usibiri takribani masaa 32 hadi 72, hapa kipimo ni chako wewe. Kama ililowa kidogo tuu basi masaa 32 yatatosha kabisa, ila kama ililowa sana, basi hakikisha ikae masaa 72. TUNAJUA UTAKUWA UNAHAMU YA KUIWASHA AU KUITOA KABLA, ILA KUMBUKA NI MUHIMU IKAUKE NDANI KABISA, Hivyo vumilia.
Tunajua baada ya hatua hizo zote utakuwa unasubiria kwa hamu kuiwasha tena. Hadi sasa itakuwa imekauka vizuri ndani, ukiiwasha tunategemea itawaka bila tatizo lolote kama ulifuata hatua zote kwa usahihi.
MAMBO MUHIMU YA KUFAHAMU
Njia hii inategemea bahati na uharaka wako katika kuondoa simu na kuizima baada ya kuwa katika maji. Kitu muhimu na kuweza kuzima simu au tableti hiyo kabla shoti haijatokea ndani yake
Ata kama itawaka vizuri na kuweza kufanya kazi kama kawaida kuna uwezekano mkubwa sana simu hiyo kuanza kutofanya kazi vizuri baada ya kipindi kirefu kama vile mwaka mmoja hivi kutokana na madhara ya kuingiwa na maji. Kuna vitu ndani yake huwa havitakiwi kukutana na maji kabisa. Hivyo ata kama itawaka na kuanza kufanya kazi kama kawaida anza kujiandaa kununua simu nyingine.
Kama simu yako ilikuwa bado ya Dhamana, yaani Warranty basi jua dhamana hiyo imevunjika rasmi. Simu janja nyingi za kisasa zinazouzwa zikiwa chini ya dhamana ya mwaka au miaka miwili zikikupa uwezo wa kuzirudisha na kupewa mpya n.k kutoka pale uliponunua huwa dhamana hizo zinafutwa kama simu iliingia maji. Na wameweka teknolojia spesheli (water indicator) ndani ya simu hizo ambapo kama simu au tableti zikilowa huwa wakifungua ndani wanatambua.