Jeshi la polisi mkoani Geita limefanikiwa kuwauwa watu wawili wanaosadikika kuwa ni majambazi baada ya kupora na kufanya mauaji ya mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Gosbert Walwa katika eneo lake la biashara, huko Geita.
Majira ya saa 12:15 watu wanaosadikika kuwa ni majambazi walivamia duka la wakala wa vinywaji ambapo walipora fedha kiasi cha shilingi millioni moja na laki nane na bastola moja, baadaye walivamia vibanda vya huduma za fedha kwa njia ya simu na kupora fedha kiasi ambacho hakijafahamika na kufanya mauaji.
Baada ya masaa mawili kwa ushirikiano wa wananchi na jeshi la polisi, majambazi waliuwawa katika msitu wa miyenze kilomita hamsini na nane kutoka Geita mjini
Posted via Blogaway