Wakati wewe ukienda Muhimbili
kujisomea Miaka 7 ili uwe Daktari
Bingwa kuna wenzio wako Mtaani
na Mtaa umewafanya wawe
Madaktari huku wakiichambua
Biology kwa macho tu bila hata
kwenda Shule;
Kuna Wanawake wana balaa
utadhani wanatembea na Ramli ya
Mganga, usiombe awe ndo
mchuchu wako Mtagombana deile,
wanajifanya wanajua kukagua
kuliko maafisa wa TRA Makao
Makuu;
Msipoonana wiki 2 mathalani
umesafiri, ukirudi sasa ukafika ule
muda wa kupunga maruhani
utamsikia,''huko ulikoenda
uliibiwa na nani?, Mbona Jongoo
amesinyaa hivi, Utanieleza
nakwambia'', timbwili la haja,
kumbe maskini joto tu la Dar
limesababisha Bunsen Burner
imekuwa Non luminous Flame;
Mtaishi maisha yote mtu mzima
kama uko Laboratory, wana
maswali yao fyongo-fyongo tu,
utasikia ''Mbona unanukia kama
kile kisabuni cha EVA cha gesti,
leo umeamkia wapi?....Kubwa
kuliko utaambiwa ''Leo uko tofauti
sana halafu hata 'kamkojo' kako
leo kana lita chache sana,
mwanaume huridhiki weye hata
upewe kila siku''....
mmmh, yaani hadi lita wanapima
kwa macho na feeling, mweh Kama
wewe mtaalamu sana si ukasaidie
kutafuta ndege ya Malaysia
iliyopotea?, Unahamishia Biology
kwenye mahaba, watu hatupumui
kwa raha, unakaa wima-wima leo
ntaambiwa kitu gani, hukawii
kuambiwa mbona Lips zako kavu
hivi umetoka kumbusu
nani..khaaa...Utadhani umeoa
Anthropologist kumbe Banker tu!;
Shkamoo wanawake wa Dar,
Mnakata kabla ya Kona!.
Posted via Blogaway