PLANET MEDIA GROUP

Tuesday, 10 June 2014

INABOA..

UNASTAHILI VITU VIZURI DAIMA!
Acha kumpigia simu mtu ambaye
huwa hapokei simu zako au
ambaye anakupigia siku akiwa na
shida maana mtu huyo haoni
umuhimu wako na inawezekana
kuna watu wengine anaoona ni
muhimu zaidi yako....Acha
kumtumia meseji mtu ambaye
hajibu meseji zako kwa madai
yuko 'busy' sana, maana huyo mtu
kama angekua anakujali na
kukupenda hawezi kukosa japo
dakika 1 ya kukujibu kuwa 'I MISS
YOU' , " I LOVE YOU"....kama mtu
huyu ni rafiki au mpenzi wako jua
kuwa hana muda kwako ila ana
muda wa kumtumia meseji mtu
mwingine ambaye anamjali kuliko
wewe… Acha kumjali mtu ambaye
hana shukrani kwa kila
ukifanyacho kwake. . Acha kulia
kwa mtu ambaye hatambui
thamani ya machozi yako. Maana
KIUKWELI unafaa kuwa na mtu
ambaye ana furahia kuona simu
yako unapopiga, mtu ambaye
anajibu meseji zako na kupenda
kuwa karibu nawe, Mtu ambaye
anashukuru hata kwa kidogo
ufanyacho kwake, Mtu ambaye
anaogopa kukupoteza katika
maisha yake yote.


Posted via Blogaway