Bado wachezaji na benchi zima la ufundi la Man United halitakuamini kwa kilichotokea kwa mshambuliaji
wao tegemeo raia wa Sweden Zlatan
Ibrahimovic kuwa
hawezi kurejea uwanjani kwa siku za karibuni kufuatia jeraha lake la goti
alilolipata wakati wa game ya Europa
League dhidi ya Anderletch. Kwa mujibu wa mitandao ya Ulaya hususani ESPN umeripoti kuwa Zlatan Ibrahimovic kufuatia jeraha lake la goti la kulia
alilolipata atakaa nje ya uwanja hadi mwezi January 2018, kitaalam Zlatan anaumwa Anterior
Cruciate Ligament (ACL), hivyo atalazimika kufanyiwa upasuaji ambao utamchukua
muda mrefu kurudi uwanjani.
Jeraha hilo alilolipata Zlatan mastaa wenzake ambao wamewahi kukutana na tatizo
hilo wamekuwa wakikaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi 9, mfano Zouma wa Chelsea aliumia katika mchezo dhidi ya Man United 2016 lakini alilazimika kurudi uwanjani baada ya
miezi 11.
Inawezekana huo ndio ukawa mwisho wa Zlatan kuvaa jezi ya Man
United kutokana na mkataba wake kuripotiwa kumalizika
mwisho wa msimu huu, sasa haijajulikana kama staa huyo aliongeza mkataba na Man United au alikuwa ameingia makubaliano ya awali kama
hakuongeza ana asilimia ndogo ya kupewa mkataba mpya akiwa katika majeruhi na
akiwa na miaka 35.