Breaking News...!!!!!!!!!
Watu 19 dead on ze spot ajali hiyo imetokea maeneo hayo lakini
kwa bahati mbaya wakati tunafika eneo la
tuklio tayari askari wa Usalama Barabarani
walisaidiwa na Wanajeshi wa kambi ya Lugalo
walisaidia kuyaondoa magari yaliyosababisha
ajali hiyo sambamba na maiti na majeruhi.
Kwa mujibu wa abiria aliyeshuhudia ajali hiyo
kutoka gari la nyuma ya daladala iliyokuwa
ikitokea Mwenge, ajali hiyo imesababishwa na
daladala lililokuwa likitokea Tegeta ambalo
lilihama njia ya kuingia katika njia ya magari
yanayotoka Mwenge na kugongana na daladala
lililolkuwa linatoka Mwenge .
Baada ya daladala hilo la Tegeta kugongana na
lingine, lilichanika na kufumuka ubavuni na
kusababisha kumwaga abiria ambao walikuwa
katika gari hilo na kupitiwa na roli ambalo
lilikuwa ubavuni mwa daladala linalotoke
Mwenge na kuwasaga kabisa .
Kwa mujibu wa shuhuda huyo anasema kuwa
watu zaidi ya 15 walisagwa na roli hilo lakini
wengine walitupipwa mtaroni pembeni mwa
barabara. Kuna uwezekano watu waliofariki ni
zaidi ya 20 .
Maiti na majeruhi wamekimbizwa katika
hospitali ya Lugalo wakisaidia na askari jeshi
ambao walipewa amri ya kutoka kikosini na
kuwasaidia majeruhi na maiti hayo.
Kutokana na msaada mkubwa wa wanajeshi
ilidumu kwa dakika 10 kulisafisha eneo hilo na
kuondoa magari hayo na maiti pamoja na
majeruhi.
Posted via Blogaway