Leo ndio siku ya siku! Mashindano ya kombe la dunia yatang'oa nanga leo huko Brazil. Mji wa Sao Paolo kutakako fanyika sherehe za ufunguzi rasmi wa mashindano hayo na pia mechi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia, umekabiliwa na matatizo si haba ikiwemo migomo ya usafiri, usalama, na ghasia za hapa na pale. Fauka ya hayo, msisimko ni mkubwa kote duniani. Je unaona ni timu gani italinyanyua kombe mara hii?
Posted via Blogaway